Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR ataka msaada uendelee kwa wakimbizi Kyrgystan

Mkuu wa UNHCR ataka msaada uendelee kwa wakimbizi Kyrgystan

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres ambaye yuko ziarani nchini Kyrgystan ametoa wito wa kuendelea kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini humo.

Bwana Guterres ameitaka jumuiya ya kimataifa kutowasahau maelfu ya watu ambao wanakabiliwa na kujenga upya maisha yao na kusahau machafuko yaliyotokea katikati ya mwezi huu wa Juni mjini Osh kusini mwa Kyrgystan .

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo ambalo wakimbizi wengi wanarejea nyumbani, Guterres amesema dunia ilishangazwa na hali ya Kyrgystan , hivyo tusishitukizwe tena.