Ban Ki-moon ameipongeza Dr Congo kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru

30 Juni 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipongeza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo leo imeadhimisha miaka 50 ya uhuru waliounyakua kutoka kwa Wabelgiji.

Katika hafla maalumu mjini Kinshasa Ban amesema sherehe hizo ni za kihistoria na yuko nchini humo kuelezea wajibu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo na nia ya Umoja wa Mataifa ya kushirikiana na Congo kwa ajili ya hatma ya nchi hiyo. Akizungumza na Radio Okapi mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa nchi ya Congo na wajibu wake kwa Afrika na dunia kwa ujumla.

(SAUTI YA BAN)

Ban ameongeza kuwa Congo na Umoja wa Mataifa wanahistoria ndefu. Juhudi za UM nchini humo zimefanyika na kukabiliana na vikwazo, lakini maelfu ya askari wa kulinda amani na wafanyakazi wengine wa ndani na nje ya Congo wameendelea kuwasaidia watu wan chi hiyo wakati wa dhiki.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter