Maelfu waendelea kusambaratishwa na machafuko jimbo la Darfur

29 Juni 2010

Wafanyakazi wa misaada kwenye jimbo la Darfur Magharibi mwa Sudan wanasema mapigano yanayoendelea baiana ya makundi mbalimbali yenye silaha yameongezeka tangu mwezi Mai.

Familia 725 zimesambaratishwa na mapigano hayo kuanzia katika maeneo ya Jebel Mara hadi kambi ya Hassa Hissa sehemu za Zalingei, magharibi mwa Darfur. Zoezi la kuthibitisha hali hii iliyofanywa na mashirika mbalimbali ya misaada Juni 27 ni kufuatia ombi la pamoja lililotolewa na , vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID wa kuzitaka pande husika kusitisha mapigano.

Juni 24 UNAMID iliarifu watu kuuawa katika mapigano kati ya jamii za Rizeigat na Misseriya katika vijiji vya Bugulay na Tereij , kilometa 28 kusini mashariki mwa Zalingei. Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Georg Charpentier amesema kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama hasa katika miezi miwili iliyopita hakuathiri tuu raia bali pia kunalenga jamii ya wafanyakazi wa misaada kama kuendelea kutekwa kwa wafanyakazi hao, kuuawa kwa wanajeshi wa kulinda amani, utekwaji wa magari na unyang'anyi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter