Mabadiliko makubwa katika uchumi wa kimataifa yanahitajika kuleta mafanikio:UM

Mabadiliko makubwa katika uchumi wa kimataifa yanahitajika kuleta mafanikio:UM

Uwiano mkubwa katika uchumi wa kimataifa unahitajika ili kuufanya uchumi kuwa imara. Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa jamii na uchumi kwa mwaka 2010 ambayo yametolewa leo na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mfumo wa uchumi wa dunia unahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa . Na ujumbe muhimu wa ripoti hiyo ni kwamba tumeshuhudia miaka ya nyuma matatizo makubwa ya kimataifa yakijitokeza ,baa la njaa, matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa na mdororo wa kiuchumi. Yote kwa kiasi kikubwa ni kutokana na kushindwa kwa mifumo ya kimataifa ya uchumi na kasoro katika muundo wa uongozi na hasa kutokuwepo kwa uhusiano katika maeneo mengi ya utungaji wa sera.

Mkurugenzi wa uchambuzi wa sera za maendeleo wa Umoja wa Mataifa na pia mwandishi wa ripoti hiyo Rob Voss anasema ili kwenda sambamba na kushughulikia mambo yanavyokwenda hivi sasa tunahitaji mabadiliko makubwa endapo tunataka utandawazi uliotengamaa.

Na kwa hilo tunahitaji kuziweka mbele nchi zinazoendelea, kuimarisha uwezo wake wa kuunda na kutekeleza mikakati yake ya maendeleo, mabadiliko makubwa katika msaada wa uhandisi, mabadiliko ya mfumo wa biashara hna hasa kuzipa nafasi zaidi nchi zinazoendelea ,sekta zake na viwanda vyake na kutafuta mshikamano wa kimataifa katika masuala ya kifedha na mazingira. Ripoti pia inataka mabadiliko katika muundo wa fedha w kimataifa, haja ya kuwa na sheria maalumu za kifedha , mabadiliko katika akiba ya kimataifa na sheria za kulinda mifumo ya fedha wakati wa matatizo