Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel imeaswa kuepuka ukiukaji zaidi wa haki mashariki mwa Jerusalem

Israel imeaswa kuepuka ukiukaji zaidi wa haki mashariki mwa Jerusalem

Mwakilishi maalimu wa Umoja wa Mataifa Richard Falk ameitaka Israel kuzuia ukiukaji zaidi wa sheria za kimataifa Mashariki mwa Jerusalem.

Amesema haswa kuhusiana na Wapalestina wanne wanaotishiwa kupoteza haki zao za ukaazi na mipango ya meya wa eneo hilo kutaka kubomoa majengo 22 ambayo ni nyumba 89 za Wapalestina katika eneo la Silwan mashariki mwa Jerusalem. Falk amesema endapo mipango hii itatekelezwa itakiuka sheria za kimataifa na baadhi ya hatua hizo kuchukuliwa kama uhalifu wa kivita chini ya haki za kimataifa za binadamu.

Ameitaka tume ya wataalamu binafsi iliyoundwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kufuatilia hali ya haki za binadamu kwenye maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa tangu mwaka 1967, kuwa chonjo na hali hiyo.