Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaitaka Jamhuri ya Afrika ya Kati kuendelea na maandalizi ya uchaguzi

UM unaitaka Jamhuri ya Afrika ya Kati kuendelea na maandalizi ya uchaguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka pande zote nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuendelea na maandalizi ya uchaguzi wa Rais na wabunge.

Uchaguzi ambao umeahirishwa mara kadhaa. Katika ripoti yake kwa baraza la usalama kuhusu hatua zilizopigwa katika nchi hiyo iliyoghubikwa na mgogoro, Ban ameitia moyo tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuendelea na kazi yake licha ya changamoto zinazozunguka maandalizi ya uchaguzi huo unaotakiwa kuwa huru, wa haki, ulio wazi na utakaojumuisha pande zote. Awali uchaguzi ilikuwa ufanyike mwezi Aprili kasha ukazogezwa mbele hadi Mai kufuatia malalamiko ya makundi ya upinza.

Hata hivyo tume ya uchaguzi ikaahirisha tena uchaguzi huo kutokana na sababu za kiufundi.

Ban ameitaka jumuiya ya kimataifa kuendelea kuisaidia mfumo wa uchaguzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusaidia fedha katika mfuko wa uchaguzi ulioanzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo.