Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umepongeza kura ya maoni kufanyika kwa amani na utulivu Kyrgystan

UM umepongeza kura ya maoni kufanyika kwa amani na utulivu Kyrgystan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi wake nchini Kyrgyzstan wamekaribisha kura ya amani ya katiba iliyofanyika jana.

Kura hiyo imefanyika kwa amani na utulivu licha ya machafuko ya huvi karibuni. Miroslav Jenca, ambaye ni mkuu kituo cha kanda cha Umoja wa Mataifa cha diplomasia Asia ya Kati (UNRCCA), alikuwa Kyrgyzstan wakati wa kura hiyo ambayo imefanyika baada ya machafuko ya kikabila baina ya Wakyrgy na Wauzbek ambayo yalizuka kusini mwa nchi hiyo kwenye miji ya Osh na Jalalabad na miji mingine mapema mwezi huu.

Machafuko hayo yaliwafanya watu 300,000 kuwa wakimbizi wa ndani na wengine 100,000 kukimbilia nchi jirani ya Uzbekistan. Wengi wa wakimbizi hao wa ndani na nje wamearifiwa kuanza kurejea katika maeneo yao taku wiki iliyopita.