Wananchi wa Burundi leo wamepiga kura katika uchaguzi wa Rais

Wananchi wa Burundi leo wamepiga kura katika uchaguzi wa Rais

Wananchi wa Burundi leo wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais kukiwa na mgombea mmoja pekee katika kiti hicho.

Hii ni baada ya upinzani kuwaondoa wagombea wake na kumuacha Rais wa sasa Pierre Nkurunziza akiwa mgombea pekee.

Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu serikali na kundi la mwisho la waasi FNL kutia saini mkataba wa amani na kukubali kushiriki katika mchakato wa kisiasa nchini humo. Je uchaguzi wa leo umekwenda vipi? Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga amefuatilia kwa kina na hii hapa taarifa yake.

(RIPOTI KIBUGA)