Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi G20 wanasema bado kuna changamoto katika kufufua uchumi

Viongozi G20 wanasema bado kuna changamoto katika kufufua uchumi

Viongozi wa G20 kwenye mkutano mjini Toronto wameahidi kupunguza madeni ya serikali kwa nusu ifikapo 2013.

Hata hivyo kutokana na kutokuwepo kwa uwiano wa kuchipuka tena kwa uchumi, wameruhusu kila nchi kuwa na kasi yake katika kurejesha uchumi kwenye hali ya kawaida.

Taarifa ya kufunga mkutano huo inasema bado kuna changamoto kubwa, wakati uchumi unaanza kuchipuka tena, ukuaji unatofautiana na hauko imara. Ukosefu wa ajira katika nchi nyingi bado uko kwenye kiwango kisichokubalika na athari zake watu wanazihisi bado.