Ban ameyataka mataifa tajiri kutimiza ahadi zake kwa mataifa masikini

28 Juni 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyatolea wito mataifa tajiri kutimiza ahadi ya kuzifadhili nchi zinazoendelea katika juhudi zake za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ban ametoa wito huo jana kwenye mkutano wa mataifa yaliyoendelea kiuchumi G20 uliofanyika mjini Toronto Canada. Ameyataka mataifa hayo kuwekeza katika nishati safi na uchumi unaojali mazingira katika moja ya juhudi za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Amesema hatari ya kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa inakua kila siku, jinsi tunavyochelewa ndivyo tutakavyolipa gharama kubwa. Ban ameshiriki mkutano huo wa siku mbili ili kuchagiza viongozi wa dunia kujikita katika kuziinua nchi zinazoendelea licha ya mdororo wa uchumi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter