Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na EU kusaidia maeneo yaliyoathirika na ukame ukanda wa Sahel

FAO na EU kusaidia maeneo yaliyoathirika na ukame ukanda wa Sahel

Wakati huu ambao tatizo la chakula linaongezeka katika eneo la Sahel na kuwaweka mamilioni katika hatari ya baa la njaa, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limeanza kugawa mbegu bora kwa wakulima nchini Burkina Faso.

Hatua hiyo ni sehemu ya operesheni inayifadhiliwa na muungano wa Ulaya(EU) ambayo imetoa euro milioni 18 kuwasaidia wakulima laki moja. Kwa mujibu wa kitengo cha FAO cha mfumo wa kutoa tahadhari na taarifa , hali ya chakula inatia mashaka katika sehemu za Sahel ambako zaidi ya watu milioni 10 wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.

Nchini Burkina Faso mvua za msimu kutonyesha kama ilivyotarajiwa imesababisha kushuka kwa uzalishaji wa chakula mwaka 2009 kwa asilimia 17. Operesheni hiyo inayofadhiliwa na FAO itaboresha usalama wa chakula kwa nyumba zaidi ya 860,00 na watu zaidi ya milioni sita. Lengo ni kuongeza uzalishaji wa chakula kwa kutumia mbegu zilizoboreshwa kuwapa wakulima wanaohitaji