Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la ajira kwa watoto kimataifa inaiweka biashara pabaya:ILO

Tatizo la ajira kwa watoto kimataifa inaiweka biashara pabaya:ILO

Matatizo ya kifedha na kiuchumi yanaongeza hatari kwamba ajira ya watoto huenda ikaongeza kasi ya kuingia kwao katika ulimwengu wa biashara.

Shirika la kazi duniani ILO limeowaonya viongozi wa biashara walokusanyika hapa New York kwa ajili ya mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa wa Global Compact, kwamba matatizo ya kifedha, kiuchumi na ajira ynaongeza shinikizo jipya ambalo linaweza kusababisha wafanyakazi watoto kuingia katika mfumo wa kimataifa wa ajira hiyo na hasa kwenye biashara.

Mkurugenzi wa ILO wa mpango wa kimataifa wa kutokomeza ajira ya watoto Constance Thomas amesema kwa makampuni kujilinda kutokana na madai ya kufanya ajira ya watoto lazima waelewe ni vipi vitendo vyao vinaweza kuathiri haki za watoto na inapowezekana kushirikiana na serikali, wafanyakazi na jumuiya za kijamii kushughulikia kiini cha tatizo ambalo litawafanya kujihusisha na ajira za watoto.

Inakadiriwa kuwa watoto milioni 215 bado wamekwama kwenye ajira ya watoto kote duniani.