Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la utapia mlo limefurutu ada nchini Niger: UNICEF na WFP

Tatizo la utapia mlo limefurutu ada nchini Niger: UNICEF na WFP

Ripoti ya utafiti wa lishe ya watoto nchini Niger iliyotolewa leo inasema hali ya lishe kwa watoto nchini Niger imeshuka sana katika miezi 12 iliyopita.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wameitaka jumuiya ya kimataifa kukusanya fedha zinazohitajika ili kuwalinda watoto hao na kuwatibu wanaoumwa.Kiwango cha kimataifa cha utapia mlo nchini Niger kimefikia asilimia 16.7 kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Kiwango hicho kimepindukia hata kiwango cha tahadhari ambacho ni asilimia 15 na kile cha asilimia 12.3 kilichoshuhudiwa mwaka jana nchini humo. Jeremy Hartley ni msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA JEREMY)