UNHCR imeruhusiwa kuanza tena shughuli zake Libya baada ya kutimuliwa

UNHCR imeruhusiwa kuanza tena shughuli zake Libya baada ya kutimuliwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeruhusiwa kuanza tena sehemu ya shughuli zake nchi Libya baada ya mazungumzo na serikali ya Libya kuhusu uamuzi wa serikali kulitimua nchini shirika hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Adrian Edward majadiliano na serikali ya Libya juu ya hatma ya mipango ya shughuli za shirika hilo yataanza hivi karibuni.

UNHCR pia imeiomba serikali ya Libya kupata ukweli wa madai yaliyotolewa awali kwamba mwakilishi mmoja wa shirika hilo alikuwa akiwapa wakimbizi hadhi kwa kubadilishana na ngono. Mapema mwezi huu serikali mjini Tripol ililitaka UNHCR kufunga ofisi zake na kufungasha virago.