Idadi kubwa ya wakimbizi wanarejea nchini Kyrygystan kwa hiyari:UNHCR

25 Juni 2010

Maafisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wamewatembelea wakimbizi wa Kyrgystan wanaorejea nyumbani kwa idadi kubwa kutoka nchini jirani ya Uzbekstan.

Wakimbizi hao wanarejea katika miji ya Osh na Jalalabad. Kwa mujibu wa serikari ya Kyrygystan wakimbizi 70,00 wamesharejea nyumbani hadi sasa na wakati huohuo wakimbizi wa ndani nao wanarejea katika makazi yao. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN)

Adrian ameongeza kuwa wanawaona watu wengi wakienda kuishi na baadhi ya familia katika maeneo ya jirani na hivyo kuongeza mrundikano na haja ya msaada zaidi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter