Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juni 26 ni siku ya kimataifa kupinga mihadarati na usafirishaji haramu

Juni 26 ni siku ya kimataifa kupinga mihadarati na usafirishaji haramu

Kila mwaka Juni 26 huadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu.

Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wakati dunia ikiwa katika maandalizi ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia hapo September ni lazima kutambua moja ya vikwazo vya maendeleo vinavinavyochangiwa na matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema ni wakati wa kufikiria afya sio mihadarati. Matumizi ya dawa hizo yanaleta changamoto kubwa za kiafya, kwani matumizi ya mihadarati kwa kutumia sindano yanaongoza kwa maambukizi ya virusi vya HIV.  Katika baadhi ya nchi matumizi ya heroin na HIV vimefika hatua mbaya. Mihadarati pia amesema ni tishio kubwa kwa mazingiramfano kilimo cha coca. Na biashara ya dawa hizo inavuruga mfumo wa utawala, taasisi na mshikamano wa jamii.

Hivi karibuni takwimu za Afrika ya Magharibi na Amerika ya Kati zimedhihirisha ni jinsi gani biashara na usafirishaji haramu wa mihadarati unavyoweza kuwa tisho kwa usalama. Ban amezitaka serikali zote kutimiza wajibu wao na kuridhia mkataba wa UM wa kupinga uhalifu wa kimataifa.