Wahalifu wa uharamia sasa kukabiliwa na mkono wa sheria nchini Kenya

25 Juni 2010

Serikali ya Kenya imewaambia maharamia sasa imetosha kwa kufungua mahakama maalumu Shimo la Tewa mjini Mombasa ili kuendesha na kuhukumu kesi za washukiwa wa uharamia.

Uharamia umekuwa ni tatizo kubwa katika mwambao wa Somalia na pwani ya bahari ya Hidi, meli nyingi za kitaifa na kimataifa zikitekwa, watu kupoteza maisha na kulifanya tatizo hilo kuwa ni la kimataifa.

Kwa msaada wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC, serikali za Ujerumani, Ufaransa, Marekani na Canada hadi sasa washukiwa zaidi ya 100 wanashikiliwa na 18 wameshahukumiwa. Kupata undani wa shughuli za mahakama hiyo mpya Flora Nducha amezungumza na msemaji wa polisi nchini Kenya Erick Kiraithe

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter