Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM DR Congo ameeleza mafanikio na changamoto nchini humo

Mwakilishi wa UM DR Congo ameeleza mafanikio na changamoto nchini humo

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema ingawa sehemu kubwa ya nchi hiyo hivi sasa ina kiasi Fulani cha amani lakini bado kuna changamoto.

Amesema miongoni mwa changamoto zilizosalia zipo sana kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambalo limeghubikwa na machafuko. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kinshasa mwakilishi huyo Alan Doss amesema "naondoka Congo nikiwa na hisia za kuridhika kwamba tumefanikisha mengi pamoja, lakini najua kwamba bado kuna changamoto nyingi za kukabiliana nazo."

Mengine ni kuweza kuwashawishi maelfu ya waasi wakiwemo wa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) ambapo 2,300 wamerejea Rwanda na askari wengi watoto wameweza kujiunga tena na familia zao. Amesema haya yote yamewezekana kwa ushirikiano mkubwa wa serikali ya Congo na watu wake.

Lakini pia amesema pamoja na mafanikio hayo kwa miaka miwili na nusu aliyokuwa nchini humo, changamoto ya vita hususan jimbo la Kivu mashariki mwa nchi hiyo na baadhi ya sehemu za jimbo la Orientale province, bado inatia hofu.