Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria na ukiukaji wa haki ni kikwazo cha vita dhidi ya ukiwmi:UNDP&UNAIDS

Sheria na ukiukaji wa haki ni kikwazo cha vita dhidi ya ukiwmi:UNDP&UNAIDS

Tume maalumu ya kimataifa ya ukimwi na sheria imezinduliwa hii leo kwa lengo la kushirikiana na masuala ya sheria.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya ukiwmi UNAIDS na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, inasema karibu miaka 30 tangu kuzuka kwa ugonjwa wa ukimwi, kuna nchi nyingi ambazo mazingira hasi ya kisheria yanakuwa kikwazo cha mapambano dhidi ya ukimwi na kuwaadhibu badala ya kuwalinda watu.

Lengo la tume hiyo mpya ni kuongeza uelewa wa athari za mazingira ya kisheria katika vita dhidi ya ukimwi. Na kikubwa ni kujikita na kuangalia jinsi gani sheria na utekelezaji wa sheria hizo unaweza kusaidia badala ya kuzuia mapambano dhidi ya ukimwi.

(SAUTI HELEN CLARK)