Skip to main content

Mchakato wa maandalizi ya uchaguzi ujao Afghanistan hauridhishi:UM

Mchakato wa maandalizi ya uchaguzi ujao Afghanistan hauridhishi:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan leo amerelezea kutoridhishwa kwake na mchakato wa kuwapata wagombea wa uchaguzi ujao wa bunge nchini humo.

Stephan de Mistura amesema kamati ya uteuzi ingekuwa imefanya juhudi zaidi kufikia sasa hivyo hajaridhika. Uchaguzi wa bunge unatarajiwa mwezi Septemba na anasema hadi sasa mchakato hauajazaa matunda yaliyotarajiwa.

Orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi huo wa Septemba 18 ambao utakuwa ni kwa mara ya kwanza taasisi za Afghanistan zinaendesha uchaguzi wake wameshatangazwa. Kati ya wagombea 2577, 13 wanaonekana kutolewa kwenye orodha ya walio na uhusiano na makundi haramu yenye silaha.

Mchujo wa wagombea ulifanyika kwa ombi lao na uliendeshwa na wizara ya mambo ya ndani, na ile ya ulinzi na usalama. Kwa sheria za uchaguzi za Afghanistan taarifa hizi zilipitishwa na taasisi za uchaguzi za nchi hiyo, tume huru ya uchaguzi IEC na tume ya malalamiko ya uchaguzi ECC kwa ajili ya hatua kuchukuliwa.