Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 90 ya dunia sasa imeunganishwa na mtandao wa sumu za mkononi

Asilimia 90 ya dunia sasa imeunganishwa na mtandao wa sumu za mkononi

Taarifa mpya zilizotolewa leo na jumuiya ya kimataifa ya mawasiliano ITU zinaonyesha kumekuwa na ongezeko la waliojiandikisha kwa matumizi ya mtandao wa simu za mkononi bilioni 1.9 kati ya mwaka 2006 na 2009 duniani kote.

Bilioni 1.6 kati ya hao wanatoka katika nchi zinazoendelea ikilinganishwa na milioni 300 kutoka nchi zilizoendelea. Katika nchi zinazoendelea zaidi ya nusu ya nyumba za vijijini hivi sasa wana simu za mkononi.

Uchina na India ndio zinaongoza duniani zikiwa na zaidi ya asilimia 90 ya vijiji vyake vina mawasiliano na hiyo ni asante kwa simu za mkononi.