Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa ripoti mchanganyiko kuhusu hatua za kufikia malengo ya milenia

UM umetoa ripoti mchanganyiko kuhusu hatua za kufikia malengo ya milenia

Ripoti ya mwaka huu kuhusu hatua iliyopigwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia inasema takwimu za vifo vya kina mama na watoto zitawachagiza viongozi wa mataifa manane tajiri G8 watakaokutana wiki hii kulipa kipaumbe cha kwanza suala hilo.

UN issues mixed report card on progress towards Millennium Development GoalsKwa mujibu wa tathimini ya Umoja wa Mataifa ya hatua zilizopigwa katika malengo manane ya maendeleo ya milenia ambayo imetolewa leo, idadi ya vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano imeshuka kutoka milioni 12.6 mwaka 1990 hadi milioni 8.8 mwaka 2008, ikienda sambamba na vifo vya kina mama ambavyo

vimepungua kutoka 100 katika kila wanawake 1000 na kifikia 72 mwaka 2008. Lakini ripoti hiyo inasema hatua zinasuasua katika lengo la nne la kupunguza theluthi mbili ya vifo vya utotoni ifikapo 2015, kwani mamilioni ya watoto wanaendelea kufa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kwa muda mrefu afya ya mama na mtoto imekuwa katika ajenda ya juu kwenye malengo ya milenia na kina mama bado wanapoteza maisha kila siku ingawa sasa huduma zimeimarika ukilinganisha mjini na vijijini. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linasema huu ni mwaka muhimu sio tuu kuhusu malengo ya milenia bali kutakuwa na mkutano mkubwa September. Cecile Mollinet ni mkurugenzi wa UNDP

(SAUTI YA  MOLLINET)