Kilimo cha coca kinapungua Colombia lakini kinaongezeka Peru:UM

Kilimo cha coca kinapungua Colombia lakini kinaongezeka Peru:UM

Kilomo cha malighafi inayotengeneza dawa za kulevya aina ya cocaine kimepungua kwa kiasi kikubwa nchini Colombia.

Nchi hiyo ndio imekuwa ikiongoza duniani kwa kuzalisha coca, lakini hali katika nchi jirani ya Peru bado inatia hofu kwani kiasi cha narcotics inayolimwa nchini humo inaongezeka kila siku imesema ripoti ya ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na dawa na uhalifu (UNODC). Kwa ujumla utafiti wa shirika hilo kuhusu mazao unaonyesha kiwango cha coca kinacholimwa katika nchi nne za Amerika ya Kusini Bolivia, Colombia, Equador na Peru kimepungua kwa asilimia 5 kutoka ekari 167,000 mwaka 2008 hadi ekari 158,000 mwaka jana wa 2009.

Na Colombia pekee kilimo cha coca kimepungua kwa asilimia 16 na kufikia ekari 68,000. UNICOD inasema sera mpya za dawa zilizopitishwa na serikali ya Colombia katika miaka michache iliyopita pamoja na ullinzi mkali na maendeleo vimesaidia.Uzalishaji wa Cocaine nchini Colombia umepungua kwa tani 410 ikiwa ni asilimia tisa kila mwaka.

Hatua ya Colombia kupinga ulimaji wa coca na uzalishaji wa cocaine umekwenda sambamba na sera za kupinga usafirishaji haramu wa dawa hizo. Mwaka jana 2009 kiwango cha cocain kilichokamatwa Colombia ni tani 200 ambazo ni kiasi kikubwa katika uzalishaji wa dawa hizo.