Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo bora wa kilimo utasaidia katika kupunguza tatizo la chakula:UM

Mfumo bora wa kilimo utasaidia katika kupunguza tatizo la chakula:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika haki ya chakula, Olivier De Shutter amesema serikali na mashirika ya kimataifa yaanahitaji kuboresha mifumo ya kilimo haraka ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuokoa mazingira.

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha matokeo ya utafiti kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu mfumo bora wa kilimo unaofanyika mjini Brussels. Mbali ya wataalamu 25 mashuhuri wa kilimo duniani mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa ameitaka jumuiya ya kimataifa kufikiria upya sera za kilimo zilizopo na kuziboresha katika misingi ya kilimo cha kisasa.

Tanzania kwa mfano katika mikoa ya Sinyanga na Tabora ilikuwa inajulikana kama jangwa la nchi hiyo lakini kutokana na mbinu mpya za kilimo zimesaidia ekari 350,000 za ardhi kuboreshwa kwa kilimo katika miongo miwili na faida kwa kila nyumba imeongezeka kiasi cha dola 500 kwa mwaka.