Ujenzi mpya baada ya kimbunga Nargis una hatihati Myanmar:OCHA

22 Juni 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema miaka miwili baada ya Myanmar kukumbwa na kimbunga Nargis kilichouwa watu 140,000 na kuwaacha wengine milioni 3 bila makao, juhudi za kuwasaidia watu hao na ujenzi mpya ziko katika hatihati kutokana na ukosefu wa fedha.

OCHA inasema kati ya dola milioni 691 zilizoombwa na Umoja wa Mataifa ni dola milioni 108 tuu zilizopatikana na hivyo kuacha pengo la dola milioni 510. Zaidi ya watu laki tano bado wanahitaji msaada wa malazi na kujikimu kimaisha.

OCHA inasema msaada zaidi wa kimataifa unahitajika kukabiliana na upungufu wa chakula, utapia mlo, mfumo wa afya, masuala ya haki za binadamu, umasikini na migogoro katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Bishow Parajuli ni mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo

(CLIP MYANMAR)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter