Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel imeutaka UM kusitisha mpango wa uchunguzi wa boti ya flotilla

Israel imeutaka UM kusitisha mpango wa uchunguzi wa boti ya flotilla

Serikali ya Israel imeuomba Umoja wa Mataifa kusitisha mipngo ya uchunguzi wa kimataifa dhidi ya shambulio la boti ya flotilla.

Ombi hilo limekuja baada ya waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak kukutana jana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hapa mjini New York. Umoja wa Mataifa uliagiza kufanyika uchunguzi wa kina baada ya wanajeshi wa Israel kuvamia boti sita zilizokuwa na msaada wa kibinadamu wa kupeleka Gaza, watu kadhaa waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika tukio hilo lililotokea mwezi Mai mwaka huu.

Ban alisisitiza kuwa uchunguzi wowote utakaofanywa na Israel na Palestina lazima uzingatie viwango vya kimataifa, uwe huru na wa haki.