Skip to main content

Suala la Somalia ni changamoto lakini kwa pamoja tutakabiliana nayo:Mahiga

Suala la Somalia ni changamoto lakini kwa pamoja tutakabiliana nayo:Mahiga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hivi karibuni amemteuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa kuwa mwakilishi wake nchini Somalia.

Balozi Agustine Mahiga ameiwakilisha Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu na pia ameshawahi kufanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambako amehusika sana na masuala ya kuielewa migogoro na hatma ya wakimbizi.

Mahiga anaenda kuchukua nafasi ya Ahmedou Ould-Abdallah mwakilishi wa sasa anayemaliza muda wake. Pamoja na pilika nyingi balozi Mahiga amempa fursa Flora Nducha wa idhaa hii kunena naye machache kuhusu changamoto atakazokabiliana nazo katika jukumu lake jipya.