Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan warejea nyumbani kwa msaada wa UM

Maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan warejea nyumbani kwa msaada wa UM

Wakimbizi takribani 70,000 wa Afghanistan wamerejea nyumbani katika kipindi cha mwaka huu.

Hii ni ishara kwamba idadi kubwa ya wale waliokimbia machafuko sasa wanaimani kuwa wanaweza kuishi nchini kwao licha cha matatizo ya kiusalama na changamoto za kiuchumi na kijamii. Haya ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo pia linasema kasi ya wanaorejea nyumbani imeongezeka katika wiki za karibuni na kufikia idadi ya 806 kwa siku. Shirika hilo linasema mara nyingi idadi ya wanaorejea hupanda katika kipindi cha mwezi wa Mai na Agosti.

UNHCR inasema Katika miezi ya karibuni wakimbizi wanaorejea wamebaini fursa za kiuchumi, hali mbaya ya usalama Pakistan, na fursa za ajira katika baadhi ya majimbo ya Afghanistan ambavyo vimekuwa chahu ya wengi kutaka kurejea nyumbani.