Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hadhi ya baraza la haki za binadamu itapimwa kutokana na mafanikio katika jamii

Hadhi ya baraza la haki za binadamu itapimwa kutokana na mafanikio katika jamii

Mafanikio na hadhi ya baraza la haki za binadamu vitapimwa sio kwa taarifa inazotoa, idadi ya maazimio inayopitisha bali ni kwa kiasi gani linaweza kuleta mabadiliko katika jamii.

Kauli hiyo ya ushauri imetolewa na Rais mpya wa baraza la haki za binadamu balozi wa Thailand. Ameliambia baraza hilo kwamba kimsingi linajukumu kubwa la kutumikia jimbo lake ambalo ni watu walio na kiu kubwa ya kulindwa na haki za binadamu, watu ambao haki zao zinakiukwa kila siku. Amesisitiza kwamba ataongozwa na masuala mengi muhimu.

Moja ni hadhi na utendaji wa baraza hilo, na pili haja ya kuimarisha majadiliano muhimu na mtazamo wa pamoja katika kupigia upatu na kulinda haki za binadamu.  Balozi Phuangketkeow amesema kwamba wakati baraza la haki za binadamu linafanya tathmini , kutakuwa na haja ya kuwepo na ubunifu wa aina fulani katika kutumia zana zilizopo kuimarisha uwezo wakekatika kukabiliana na masuala ya haki za binadamu