Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji kwa wasiojiweza ni muhimu kwa uchumi na kutimiza malengo ya milenia:UM

Uwekezaji kwa wasiojiweza ni muhimu kwa uchumi na kutimiza malengo ya milenia:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa nchi zilizoendelea kiviwanda na mataifa yanayoendelea kujikita katika maendeleo, uchumi unaojali mazingira na mahitaji ya wsiojiweza katika mikakati ya kuchipua uchumi.

Ban amesema ninachagiza msaada wa mikakati ambayo itasaidia kurejesha katika hali yake uchumi wa kimataifa, masuala ya mazingira na kufikia malengo ya milenia(MDG'S). Kauli hii imeandiwka katika barua ya Ban kwa viongozi wa kundi la nchi 20 tajiri.

Viongozi wa mataifa mataifa hayo 20 watakutana Toronto Canada tarehe 26 na 27 mwezi huu na baadaye Novemba watakuwa Seoul Jamhuri ya Korea. Na mkutano wa Toronto utafuatiwa na mkutano wa mataifa nane tajiri duniani G8 ambayo ni Canada, Ufaransa, Marekani, Uingereza, Urusi, Ujerumani, Japan na Italia.