EAC imeridhia muundo wa sheria za mtandao kuinua uchumi na uwekezaji
Mkutano wa siku tatu wa kitengo cha utendaji cha jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuhusu sheria za matumizi ya mtandao umemalizika leo mjini Kigali Rwanda.
Kwenye mkutano huo wajumbe walijikita katika kutekeleza muundo wa sheria za mtandao zilizopitishwa hivi karibuni na baraza la jumuiya ya Afrika ya Mashariki, lililohusisha mawaziri wa usafiri, mawasiliano na hali ya hewa. Muundo huo ulitayarishwa kwa msaada wa UNCTAD ambapo maafisa wa serikali wa jumuiya ya afrika Mashariki watayapa uzito masuala ya kisheria kama haki ya umilikaji wa nyumba, ushindani wa kibiashra, masuala ya kodi za mtandao na usalama.
Nchi wanachama wanafikiria kurudhia sheria hizo za mtandao ambazo ni muhimu kwa kutekeleza huduma za kiteknolojia za serikali na kuongeza biashara na uwekezaji wa kikanda.