Skip to main content

Walinda amani wa UNAMID kutoka Rwanda wauawa Magharibi wa darfur

Walinda amani wa UNAMID kutoka Rwanda wauawa Magharibi wa darfur

Taarifa kutoka Darfur zinasema wanajeshi watatu wa kulinda amani wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID, wameuawa kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan.

Mwanajeshi mwingine ambaye hakuwa na sare amejeruhiwa vibaya wakati kituo cha UNAMID Mgharibi mwa Darfur kiliposhambuliwa mapema leo. Washambuliaji watatu pia waliuawa wakati askari wa UNAMID walipojibu mashambulizi.

Wanajeshi wote waliouawa ni raia wa Rwanda, na jana jioni baadhi ya walinda amani waliokuwa wakishika doria waliarifu kusumbuliwa na kundi lililojitenga la SLA-AW. Hata hivyo UNAMID bado haijithibitisha endapo matukio hayo mawili yanaingiliana.

(SAUTI YA KEMAL SAIKI)