UNCTAD imewataka washirika wa biashara Afrika kulisaidia bara hilo katika usafirishaji nje wa bidhaa zake

UNCTAD imewataka washirika wa biashara Afrika kulisaidia bara hilo katika usafirishaji nje wa bidhaa zake

Ripoti mpya kuhusu mfumo wa biashara Afrika inaonya kuwa kukuwa kwa maingiliano ya biashara na nchi kubwa zilizoendelea zikiwemo China, India, na Brazil, hakujalisaidia bara hilo kusafirisha bidhaa zinazoliongezea faida.

Katibu Mkuu wa UNCTAD Supachai Panitchpakdi, amesema hata hivyo mfumo wa biashara na uwekezajipande wa kusini unaimarisha mfumo wa muda mrefu ambapo nchi za Afrika zinasafirisha nje bidhaa za kilimo, madini, chuma, na mafuta yasiyosafishwa na zinaingiza bidhaa zilizokwisha tengenezwa.