Skip to main content

Siku ya kimataifa ya wakimbizi: kauli mbiu ya mwaka huu ni "nyumbani"

Siku ya kimataifa ya wakimbizi: kauli mbiu ya mwaka huu ni "nyumbani"

Siku ya kimataifa ya wakimbizi huadhimishwa kila mwaka Juni 20, na kauli mbiu ya mwaka huu ni "nyumbani" na hii ni kwa kutambua haja ya wakimbizi milioni 40 kote duniani.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa wakimbizi Antonio Guterez UNHCR iko katika juhudi kubwa ya kuwarejesha kwa hiyari nyumbani mamilioni ya wakimbizi lakini ripoti ya mwaka huu inaonyesha idadi ya wakimbizi kutokana na vita na mizozo ya kisaisa inayoendelea kote duniani imeongezeka, na wale wanaorejea nyumbani kwa hiyari idadi imekuwa ndogo sana kuliko wakati mwingine wowote katika miongo miwili iliyopita.

Waswahili husema aisifiaye mvua imemnyeshea. Je maisha ya ukimbizi yakoje? Mmoja kati ya walioonja maisha hayo baada ya wazazi wake kukimbia vita ametutembelea katika studio zetu.

Na hizo ndio ndoto za wengi siku moja kuishi kama watu wa kawaida nao kuweza kuwasaidia wenzao. Lakini kwa mujibu wa UNHCR tatizo kubwa hivi sasa ni kupata nyumba mpya za kuwaruhusu wakimbizi kuanza upya maisha yao na kuwa na mahali pa kupaita nyumbani kwani wanaamini kuwa na ujumbe wao kwa mwaka huu "mmechukua nyumba zetu lakini hamuwezi kuchukua maisha yetu ya baadaye" hivyo UNHCR katika kuadhimisha siku hiyo inapiga chepuo kubwa ya kukufanya ufikirie inamaanisha nini kuwa wakimbizi kwa mamilioni ya watu, Nezia anapata picha gani