Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imefungua ofisi kaskazini mwa Sri Lanka kulikoathirika na mapigano 2008

WFP imefungua ofisi kaskazini mwa Sri Lanka kulikoathirika na mapigano 2008

Shirika la mpango wa chakula duniani limefungua tena ofisi zake eneo la Kilinochi kaskazini mwa Sri Lanka ambako kuliathirika na machafuko mwaka 2008.

Majengo ya WFP yaliharibiwa vibaya na mashambulizi ya angani na mabomu. Kwa mujibu wa msemaji wa WFP Emilia casella hivi sasa shirika hilo lina wafanyakazi katika eneo hilo na litakuwa tayari kuanza shughuli zake za kusimamia ugawaji wa chakula kwa maelfu ya watu waliosambaratishwa na mapigano hayo.

Anasema watu 128,000 wamerejea makwao na wengine 62,000 bado wako katika makambi ambapo wote walioko makambini na waliorejea nyumbani wanapata msaada wa WFP. Pia anasema watoto 300,000 wanapata mlo shuleni nchini Sri Lanka. Mbali ya watoto WFP inatoa chakula kwa kina mama wajawazito 275,000 na wanaonyonyesha.