Skip to main content

Mlipuko mpya wa Surua mashariki na kusini mwa Afrika unatia hofu: WHO na UNICEF

Mlipuko mpya wa Surua mashariki na kusini mwa Afrika unatia hofu: WHO na UNICEF

Shirika la Afya duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wanasema wanatiwa hofu na ongezeko jipya kwa ugonjwa wa surua mashariki na kusini mwa Afrika.

Mashirika hayo yanasema hali hii inazifanya juhudi zilizofikiwa kupunguza vifo hususan vya watoto kutokana na ugonjwa huo kuwa katika hatari ya kubadilika. Tangu katikati ya mwezi huu wa Juni 2010 mlipuko wa surua umewaathiri zaidi ya watoto 47,907 katika nchi 14.

Mlipuko huo umeshasababisha vifo 731 na nchi zilizokumbwa karibuni na mlipuko huo ni Malawi, Msumbiji na Zambia. Christiane Berthiaume ni msemaji wa UNICEF