Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO imetoa mwongozo mpya wa kuimarisha matumizi ya dawa za watoto

WHO imetoa mwongozo mpya wa kuimarisha matumizi ya dawa za watoto

Shirika la afya duniani WHO limetoa mwongozo wa kwanza mpya na wa aina yake kwa ajili ya matumizi ya dawa za watoto. Mwongozo huo unatoa maelezo ya jinsi ya kutumia zaidi ya aina 240 za dawa za kutibu maradhi mbalimbali kwa watoto wachanga hadi umri wa miaka 12.

Hii inamaanisha kwamba kwa mara ya kwanza wataalamu wa afya kote duniani watakuwa na taarifa zenye viwango sawa kwa ajili ya kutoa maelekezo ya kutumia , kiasi cha dawa, athari zake na dalili za matumizi ya dawa hizo kwa watoto.

Baadhi ya nchi zilianzisha mifumo na maelekezo yake kwa miaka kadhaa, na hadi sasa kulikuwa hakuna muongozo wa aina moja wa kutumia dawa za watoto kwa nchi zote.