Mkuu wa UM ametiwa moyo na hatua ya Israel kutathmini sera zake dhidi ya Gaza

Mkuu wa UM ametiwa moyo na hatua ya Israel kutathmini sera zake dhidi ya Gaza

Kumekuwa na matamko mbalimbali kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ya Israel ya kupunguza vizuizi Gaza.

Taarifa rasmi ya Umoja wa Mataifa inasema Katibu Mkuu Ban Ki-moon ametiwa moyo na serikali ya Israel kuamua kutathimini sera zake dhidi ya Gaza na anatumaini kwamba uamuzi wa leo Alhamisi wa baraza la mawaziri la Israel ni hatua kubwa katika kukidhi mahitaji ya Gaza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Katibu Mkuu amemtaka mwakilishi wake maalumu Robert Serry kuihusiha mara moja serikali ya Israel ili ifahamu zaidi kuhusu uamuzi na hatua zaid i za utekelezaji zinazohitajika. Taarifa hiyo inasema Umoja wa Mataifa unaendelea kushinikiza mabadiliko zaidi ya sera kama yalivyokubaliwa kwenye mkutano wa pande nne Quartet uliojumuisha Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, Urusi na Marekani ili misaada ya kibinadamu , bidhaa za biashara, na watu waweze kuingia na kutoka bila matatizo, jambo ambalo litasaidia ujenzi wa Gaza kufanyika.