Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Cambodia inakabiliwa na changamoto kubwa kutimiza haki kwa wote

Cambodia inakabiliwa na changamoto kubwa kutimiza haki kwa wote

Mfumo wa sheria nchini Cambodia unakabiliwa na changamoto kubwa katika kuhakikisha unatimiza haki kwa wote na hususan masikini wasiojiweza.

Hili ni hitimisho la mtaalamu binafsi wa Umoja wa Mataifa aliyekuwa katika mpango wa siku kumi nchini humo kutathimini hali ya haki za binadamuna utendaji wa mfumo wa sheria. Mtaalamu huyo Surya Prasad Subedi amesema kuna idadi kubwa ya kutisha ya watu walio mahabusu kutokana na kasoro mbalimbali za mfumo wa sheria wa nchi hiyo na kutotenda haki ni tatizo kubwa Cambodia.

Hata hivyo bwana Subedi amekaribisha kupitishwa kwa sheria mbalimbali mpya zenye lengo la kuimarisha mfumo wa sheria wa nchi hiyo. Baadhi ya mambo yaliyomtia hofu mtaalamu huyo ni pamoja na jinsi mfumo wa sheria unavyoingia uhuru wa kujieleza, fursa finyu ya kukosoa masuala ya siasa katika jamii kutokana na waandishi wengi kufunguliwa kesi na wanaharakati wa haki za binadamu kutopewa nafasi.