Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba mpya kwa wafanyakazi wa nyumbani unajadiliwa kwenye mkutano wa ILO

Mkataba mpya kwa wafanyakazi wa nyumbani unajadiliwa kwenye mkutano wa ILO

Shirika la kazi duniani ILO leo limeanza mjadala kuhusu mswada wa mkataba wa wafanyakazi wa nyumbani mjini Geneva.

ILO inasema kupitishwa kwa viwango vya kimataifa vya kazi kwa wafanyakazi wa nyumbani kutatoa fursa kwa shirika hilo kuwajumuisha katika mikakati yake wafanyakazi ambao wamekuwa nje ya miakataba yake.

Wajumbe katika mkutano huo wamesema kwamba ingawa wafanyakazi wa ndani ni jambo la linalofanyika kote duniani lakini wengi wa wafanyakazi hao hawalindi na sheria za kimataifa na hivyo kuwaacha katika hatari ya kunyanyaswa.