Skip to main content

Washikira na wadau wa afya wanazindua mipango ya 2010-2012 kutokomeza polio

Washikira na wadau wa afya wanazindua mipango ya 2010-2012 kutokomeza polio

Wadau na washirika mbalimbali wa afya leo wanazindua rasmi mipango maalumu ya mwaka 2010 hadi 2012 ya kutokomeza ugonjwa wa polio mjini Geneva.

Utokomezaji wa polio bado ni suala muhimu barani Afrika, kwani nchi 10 kati ya 15 ambazo awali zilikuwa huru kutokana na polio sasa maambukizi yamerejea tena 2009 lakini sasa zimefanikiwa kuzuia maambukizi.

Nchi hizo sasa zinashuhudia mafanikio ya kupambana na ugonjwa huo. Nigeria ni miongoni mwa nchi hizo ambapo maambukizi mapya yamepungua kwa zaidi ya asilimia 90, kutoka visa 312 wakati kama huu mwaka jana na kufikia visa vitatu mwaka huu. Na India majimbo pekee yaliyokuwa yameathirika ya Uttar Pradesh na Bihar kwa mara ya kwanza hayaripoti visa vyoyote kwa miezi sita sasa.

Mawaziri wa afya kutoka Nigeria, Afganistan, Angola na Senegal ni miongoni mwa maafisa wengine wanaohudhuria mkutano huo yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF na WHO.