Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukabiliana na mmomonyoko wa udogo ni muhimu kwa maisha ya binadamu: UM

Kukabiliana na mmomonyoko wa udogo ni muhimu kwa maisha ya binadamu: UM

Leo ni siku ya kukabiliana na tatizo la ukame duniani na maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza haja ya kuyatunza maeneo makavu ambayo ni makazi ya watu masikini zaidi ya bilioni moja na ambako kuna changamoto kubwa ya kufikia malengo ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa siku hii ya kimataifa ya kukabiliana na jangwa na ukame amesema tunapolinda na kuyatunza maeneo makavu tunaokoa mambo mengi katika wakati mmoja, tunaimarisha usalama wa chakula, tunatatua matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa, tunawasaidia masikini kutimiza ndoto zao na tunapiga hatua katika mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo ya millennia.

Ban pia amesema ukataji miti ambao husababisha jangwa ni tatizo linaloendelea. Kwa miaka 40 iliyopita maeneo mengi ya kilimo sasa yamegeuka na kuwa jangwa hayazalishi tena na mengi yametelekezwa. Ametaka kuwepo na juhudi za kimataifa na za pamoja kuhakikisha tunakabiliana na tatizo la ukame na ukataji miti unaosababisha jangwa. Siku ya kimataifa ya kupambana na ukame na jangwa huadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Juni.