Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali, wafanyakazi na waajiri waafikia viwango vipya kwa ajili ya HIV na Ukimwi

Serikali, wafanyakazi na waajiri waafikia viwango vipya kwa ajili ya HIV na Ukimwi

Serikali, wafanyakazi na waajiri wanaokutana mjini Geneva katika mkutano wa kimataifa wa kila mwaka wa Shirika la kazi duniani ILO leo wamepitisha viwango vipya vya kimataifa kwa HIV na Ukimwi.

Hili ni shirika la kwanza la kimataifa linalozingatia haki za binadamu kujikita hususan katika masuala ya Ukimwi katika mazingira ya kazi. Viwango hivyo vipya vimepitishwa kwa njia ya kura , 439 wakiunga mkono, 4 wakipinga na 11 hawakupiga kura kabisa.Hatua hii imefikiwa baada ya mjadla na majadiliano ya miaka miwili.

Hivi ni viwango vya kwanza vya kimataifa kupitishwa kisheria kwa lengo la kuimarisha mchango wa dunia katika kazi kwa kuiwezesha kuzuia virusi vya HIV, kutibu, kuwauguza na kuwasaidia na pia kuweka mipango ya kuokoa maisha na hatua za kutowabagua katika ngazi ya kazi na kitaifa. Viwango hivyo pia vinachagiza umuhimu wa ajira na miradi ya kuongeza kipato kwa wafanyakazi wanaoishi na virusi vya HIV. Dr Sophia Kisting ni mkurugenzi wa ILO katika mipango ya HIV na Ukimwi