Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMIS imewapongeza wadau wa makataba wa CPA kuunda serikali Sudan

UNMIS imewapongeza wadau wa makataba wa CPA kuunda serikali Sudan

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan (UNMIS) umewapongeza wadau wa mkataba wa amani ya Sudan (CPA) kwa kuundwa serikali mpya ya nchi hiyo.

Serikali ambayo inabeba jukumu kubwa la kutekeleza mkataba wa amani wakati wa mwaka wa misho wa kipindi cha mpito. UNMIS inatumai kwamba serikali mpya ya Sudan itaruka viunzi kwa kufikia amani ya kudumu kwa kuendesha kura ya maoni Sudan Kusini na Abyei na kutambua umaarufu wa kujadikli katika jimbo la kusini la Kordofan na Blue Nile.

Kwa maana hii UNMIS inawachagiza washirika hao wawili kusaidia kufanikisha kuundwa kwa tume za kura hizo za maoni kwa wakati Sudan Kusini na Abyei. UNMIS imerejea kutaja wajibu wake wa kuunga mkono kwa kila hali utekelezaji wa CPA na pia kusaidia pande husika katika wakati muhimu ujao wa kura za maoni kwa Wasundan.