Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa fedha wawakeka watu milioni 120 katika hatari:UNICEF

Upungufu wa fedha wawakeka watu milioni 120 katika hatari:UNICEF

Zaidi ya watu milioni 120 watakuwa katika hatari ya kupata homa ya manjano endapo kampeni kumbwa ya chanjo iliyopangwa haitofanyika katika nchi za Nigeria na Ghana.

Hii ni kwa mujibu wa kundi la uratibu wa kimataifa ICG linalohusika na ugawaji wa chanjo ya homa ya manjano. Matatizo yanayoendelea ya upungufu wa fedha yanatishia ugawaji wa kimataifa wa chanjo ya homa ya manjano na huend ikaziondoka nchi hizo mbili katika kampeni ijayo ya chanjo.

Katika miaka mitatu iliyopita kampeni Afrika ya Magharibi imewezesha watu milioni 16 kupata chanjo na hivyo kuwaepusha na hatari ya kupata mlipuko wa homa hiyo.