Vikwazo vya Israel Ukingo wa Magharibi vimepungua asilimia 20:OCHA

Vikwazo vya Israel Ukingo wa Magharibi vimepungua asilimia 20:OCHA

Idadi ya vizuizi vya barabarani vya Israel kwenye Ukingo wa Magharibi vimepungua kwa asilimia 20 mwaka jana.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa hata hivyo wanasema maeneo yaliyoimarika zadi na vikwazo hivyo ni ya katikati. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA Phillipe Lazzarini amesema masuala ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine yameimarika kwenye baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi na kuwa rahisi kutoka kaskazini kwenda kusini mwa mji.

Lakini ametaja kuwa bado hakuna mabadiliko sana inapokuja suala la kwenda maeneo ya magharibi, mashariki mwa Jerusalem au kuingia Israel. Na hali haijaimarika kabisa kuelekea mashariki na bonde la mto Jordan. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa Israel imepunguza viozuizi vya barabarani kutoka 626 hadi kufikia 505. OCHA inakadiria kwamba asilimia 26 ya Ukingo wa Magharibi limeghubikwa na jeshi na makombora huvurumishwa kutoka huko, hivyo ni vigumu kuwa na shughuli za maendeleo kama kilimo au ufugaji.