Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu limejadili ubaguzi wa rangi na migogoro

Baraza la haki za binadamu limejadili ubaguzi wa rangi na migogoro

Baraza la haki za binadamu linalokutana mjini Geneva leo limejadili masuala ya ubaguzi na athari zake.

Majadiliano hayo yamemuhusisha mwakilishi maalumu kuhusu masuala ya mifumo ya sasa ya ubaguzi wa rangi na kundi la wataalamu wanaoshughulika na watu wenye sili ya Afrika.

Katika ripoti yake mwakilishi huyo maalumu Githu Muiga amesema endapo watu hawatozingatia dalili zilizopo za ubaguzi na watu kunyimwa haki zao basi matokeo yake ni kuzuka kwa migogoro. Kwa watu wenye asili ya Afrika mambo yaliyojadiliwa ni masuala ya elimu ,afya na haki. Ameongeza kuwa migogoro, ubaguzi wa rangi, mauaji ya kulenga wageni na kutovumiliana kunaathari kubwa kwa migogoro

SAUTI YA  GITHU MUIGA)