Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wawili waasi wa Sudan leo wamejisalimisha mahakama ya ICC

Viongozi wawili waasi wa Sudan leo wamejisalimisha mahakama ya ICC

Viongozi wawili wa waasi wa Sudan wanaoshukiwa kutekeleza uhalifu wa vita kwenye jimbo la Darfur Sudan leo asubuhi wamejisalimisha kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Waasi hao ni Abdallah Banda Abakaer Nourain maarufu kama Banda na Saleh Mohammed Jerbo Jamus anayejulikana sana kama Jerbo. Waasi hao walitakiwa mahakamani tangu tarehe 27 Agosti ya mwaka 2009, wanashitakiwa kwa makosa matatu ya uhalifu wa vita wanayodaiwa kuyatekeleza wakati wa shambulio la Septemba 29 mwaka 2007.

Shambulio hilo lilifanywa dhidi ya mpango wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani nchini Sudan AMIS katika eneo la kijeshi la Haskanita na kuuwa wanajeshi 12 na kujeruhi wengine wanane. Waasi hao wanatarajiwa kusomewa mashitaka yao kwenye mahakama ya ICC kesho Alhamisi.