Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti mpya ya UNICEF inaelezea hali mbaya inayowakabili watoto Djibouti

Ripoti mpya ya UNICEF inaelezea hali mbaya inayowakabili watoto Djibouti

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNUCEF inaonyesha kuwa watoto walio wengi nchini Djibouti wanaishi katika umasikini ambao unawaweka katika hali inayotishia maisha yao.

Ripoti hiyo ni matokeo ya utafiti wa umasikini kwa watoto uliofanywa na UNICEF kwa ushirikiano na wizara ya kuchagiza maendeleo ya jamii na wanawake mwishoni mwa mwaka jana. Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Josefa Marrato anasema hali ya umasikini Djibouti inaeleza mazingira ya hatari wanayoishi watoto ambayo ynawaweka katika haki ya kunyonywa na kunyanyaswa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo watoto wawili kati ya watatu nchini Djibouti wananyimwa takribani haki moja kati ya haki za watoto ikiwemo ya kuwa na malazi, maji na usafi, kupata taarifa, lishe, elimu na afya.