Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama limetoa wito wa kutekeleza makataba wa amani Sudan

Baraza la usalama limetoa wito wa kutekeleza makataba wa amani Sudan

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza umuhimu wa kutekeleza makubaliano yote ya mkataba wa amani nchini Sudan ikiwepo maandalizi kwa wakati ya kuendesha kura ya maoni hapo mwakani.

Katika taarifa iliyosomwa na Rais wa baraza hilo balozi Claude Heller wa Mexico, baraza pia limeyataka makundi yote ya waasi kujiunga na mchakato wa amani na kuzitaka pande zote kujihusisha na majadiliano ya Doha.

(SAUTI YA HELLER )

Makubaliano ya amani yalitiwa saini 2005 baiana ya serikali na kundi la Sudan People's Liberation Movement SPLM, ili kumaliza vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Pamoja na mambo mengine mkataba huo uliandaa ratiba ambayo Sudan Kusini itafanya kura ya maoni kuamua endapo itajitenga na kaskazini mwa Sudan. Kura hiyo itafanyika Januari mwakani.